Cucumis - Huduma huria ya utafsirishaji mtandaoni
. .



Usaidizi - Tafsiri

Mawaidha machache

1 Tunaonelea ni bora utafsiri kwenda lugha yako ya kiasilia. Tafsiri tu kwenda lugha yako ya kiasili au lugha unayoweza kuizungumza vizuri
2 Heri kutafsiri vizuri kuliko kutafsiri haraka
3 Usitafsiri kila neno moja kwa moja
4 Pima maana kabla ya kutafsiri
5 Ikiwa hauna uhakika kuhusu maana ya nakala tunaonelea ni heri usiitafsiri
6 Unaweza kuanzisha majadiliano kuhusu tafsiri au kutumtumia ujumbe mtu aliyeuandika ili upate kujua vipengele zaidi
7 Usitumie vifaa vya kutafsiri moja kwa moja
8 Tilia maanani vipengele vyote, vituo, herufi kubwa ...
9 Kumbuka kuwa tafsiri zako zote zinaangaliwa na wataalamu na wasimamizi; alama zinazopatikana kutokana na kila tafsiri pia yategemea ujuzi wako wa wastani katika lugha hiyo

Sababu za kukataa tafsiri

1 Tafsiri ambayo haijamalizika
2 Kuna makosa mengi sana
3 Kutafsiri kwenda lugha isiyofaa
4 Shida ya vituo, herufi ndogo na kubwa
5 Utumizi wa kifaa cha kutafsiri moja kwa moja
6 Kazi ya purukushani

Msimamizi - Mtaalamu

Hapa kuna maelezo kanuni kwa Wataalam na Wasimamizi
1 Tafsiri zote zinapewa alama na wataalamu pamoja na wasimamizi. Wana haki zaidi na pia majukumu zaidi. Bila wao kujihusisha, hakuna tafsiri inayoweza kukubaliwa, hiyo ndiyo sababu wanatuzwa alama za bakshishi.
2 Wasimamizi na wataalamu, wakati unapoangalia (kupa alama, kubali, kataa) tafsiri fulani, unapata 1 asilimia ya alama za kutafsiri, chache zaidi 1 alama, juu zaidi 10 alama.
3 Unaweza kupata tafsiri zinazohitaji kuangaliwa kwa kubofya kwa kitu kinacholingana cha menu ya kushoto. Unaweza pia kuona kuona tafsiri zilizokataliwa na aliyeomba tafsiri. Hizo tafsiri zilizokataliwa ni nadra lakini lazima zipewe kipaumbele kwa kutathminiwa
4 Kabla ya kukubali tafsiri, hakikisha tafsiri hiyo yakaribia kuwa sawa.
5 Kwanza kabisa tafsiri lazima itii maana ya nakala asilia.Lazima iandikikwe kwa msamiati mufti na mfasiri aongeaye lugha hiyo vyema.
6 Tafsiri lazima ifwate vituo, herufi kubwa na herufi ndogo za nakala asilia. Kwa mfano ikiwa hakuna kikomo mwishoni mwa sentensi za nakala asilia, lazima kusiwe na kikomo katika nakala iliyotafsiriwa.
7 Tafsiri lazima itilie maanani kanuni mahsusi za lugha inayolengwa. Kwa mfano katika lugha ya Kihispania alama ya kuuliza swali ama alama ya mshangao iliyopinduliwa yaja kabla ya sentensi, katika Kijapani sentensi zinaisha na "。" (si na ".") na hakuna nafasi kabla ya sentensi inayofuata, n.k...
8 Kabla ya kukubali tafsiri, tazama kuwa hakuna majibu au chaguo nyingi za tafsiri katika tafsiri yenyewe kwani itaharibu uwiano kati ya nambari za herufi kulingana na lugha. Ikiwa itahitajika, hariri na songeza majibu au machaguzi ya tafsiri yasiyosadikika kwenda "Maelezo kwa mfasiri" maeneo ya hati.

Kataa au hariri?
1 Tilia maanani kiasi ya kazi iliyokamilishwa na mfasiri. Ikiwa kuna maneno machache pekee yanayohitaji kurekebishwa au kituo kuongezwa, tunaonelea ni heri uihariri tafsiri na uikubali. Hautapata alama zozote kwa kuihariri lakini utapata alama kila wakati utakapoikubali au kuikataa tafsiri.
2 Wakati kuna makosa mengi mno, tafadhali angalia profaili ya mfasiri. Ikiwa mfasiri hajaa kwa muda katika tovuti ya Cucumis.org, tafadhali mtumie ujumbe wa kibinafsi ukimweleza sababu za kuikataa tafsiri.
3 Wakati hauna uhakika, tunaonelea ni bora uanze majadiliano kuhusu tafsiri ili kuomba usaidizi kutoka wanachama wengine.