Cucumis - Huduma huria ya utafsirishaji mtandaoni
. .



Cucumis - Huduma huria ya utafsirishaji mtandaoni

Sisi ni nani?

Cucumis ni jamii ya wafasiri ambao wanashirikisha hekima zao za kilugha na wanasaidiana mtandaoni.

Ni ya nini?

Cucumis ni tovuti ambapo unaweza kupatiana nakala itafsiriwe na jamii yetu.
Unataka [tafsiri] au [kutafsiriwa]?

Inafanya kazi vipi?

Ili kutumia huduma za Cucumis, lazima uwe mwanachama aliyejisajili, unapata alama kila unapotafsiri nakala na unahitaji alama ili utupatie nakala tukutafsirie.

Ikiwa huongei lugha ya kigeni utafanyaje?

Ikiwa haujui lugha yoyote geni , tunakuruhusu kutumia cucumis kwa kukupa alama 300 kila masiku 10 (wakati tu unapoingia tovuti na wakati unapozihitaji).

Ni pesa ngapi?

Huria. Cucumis imejengwa na ile dhana ya kubadilishana huduma ya kutafsiri kwa manufaa ya wote.

Jambo gani kuhusu ubora wa tafsiri?

Tafsiri zote zinapewa alama na wataalamu pamoja na wasimamizi. Mwanachama anapandishwa cheo na kuwa "Mtaalamu" wa lugha fulani wakati anapozimaliza tafsiri nyingi za lugha fulani ambazo ni za alama iliyozidi 7/10. Ukitaka kuhakikisha tafsiri ni teule, unaweza kuuliza na ni "Mtaalamu" atakayeifanya lakini itagugarimu alama zaidi.

Mbona jina la cucumis?

Cucumis ni neno linalotafsirika kama "Mtengomaji" kutoka Latini, tunda la mviringo kama dunia, lililojaa ustawi na furaha. Kunazo lugha zaidi ya 3000 zinazozungumzwa duniani, tunatumai kuwa tuvuti hii itatusaidia kujuana.